IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Washindi wa Mashindano ya Qur’ani, Sunnah  Afrika Magharibi wazawadiwa

23:31 - October 20, 2024
Habari ID: 3479622
IQNA - Toleo la kwanza la Mashindano ya Qur'ani Tukufu na Sunnah kwa nchi Afrika Magharibi yalimalizika nchini Mauritania kwa kufanyika sherehe ambapo washindi walitajwa na kutunukiwa zawadi.

Sherehe za kufunga, zilizofanyika katika mji mkuu wa Mauritania wa Nouakchott, zilihudhuriwa na Mufti Mkuu wa Mauritania Sheikh Ahmed Ould Murabit, maafisa wa Mauritania, na wanadiplomasia wa nchi za Kiarabu na Waislamu.
Katika hotuba iliyorekodiwa, Waziri wa Masuala ya Kiislamu wa Saudia  Sheikh Abdullatif Al-Sheikh alitoa shukrani kwa Rais wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani kwa kuandaa mashindano hayo.
Al-Raqabi alisisitiza nafasi ya mashindano hayo katika kuhimiza kuhifadhi na kusoma Qur'ani na Sunnah katika ulimwengu wa Kiislamu.
Mashindano haya yaliandaliwa na Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Mauritania, kwa usaidizi na usimamizi wa Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya Saudi Arabia.
Yalikuwa na washiriki 136 kutoka nchi 16 wakishindana katika makundi makuu mawili: kuhifadhi Quran na kuhifadhi Hadithi za Mtume Muhammad (SAW_.
Majaji watano waliwatathmini washindani katika kitengo cha Quran, huku jopo jingine la wataalamu watano waliobobea katika Hadith likiwatathmini washiriki katika sehemu ya Sunnah.

3490350

Habari zinazohusiana
captcha